QUR,ANI TUKUFU na tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili- Barwani

صفحة 1

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ١

1. KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU .[1]

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ٢

2. Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;[2]

ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ٣

3. Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;[3]

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ٤

4. Mwenye kumiliki siku ya malipo.[4]

إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ٥

5. Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada.[5]

ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ٦

6. Tuongoe njia iliyonyooka.[6]

صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ٧

7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.[7]